1

TPDC yakabidhi fedha za Madawati Kinyerezi-Dar

1Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Bw. Raymond Mushi (kulia) akipokea mfano wa hundi ya Shilingi 7,440,000 kwa ajili ya kununulia Madawati katika Shule ya Msingi Zimbili, Kinyerezi kutoka kwa Meneja Mawasiliano wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Marie Msellemu (Kushoto) kwa niamba ya Mkurugenzi wa Mtendaji wa TPDC.

2

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Bw. Raymond Mushi akitoa neno la Shukurani mara baada ya kupokea hundi ya Shilingi 7,440,000 kutoka TPDC.

3

Meneja Mawasiliano – TPDC, Marie Msellemu akizungumza katika halfa ya kukabidhi hundi ya Shilingi 7,440,000 kwa ajili ya kununulia Madawati ya Shule ya Msingi Zimbili, Kinyerezi Jijini Dar es Salaam leo, wengine ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Bw. Raymond Mushi (wa pili kulia) na Diwani wa Kinyerezi, Greyson Selestine (kushoto).

No.1(1)

TPDC yaongeza kiwango cha uzalishaji gesi kwa kuzindua mtambo mpya wa Songo Songo

Kwa mara nyingine Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limeongeza kiwango cha uzalishaji gesi nchini kwa kuzindua mtambo mpya uliopo Songo Songo. Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio katika uzinduzi huo Kisiwani Songosongo alisema Kiwanda hicho kinapokea gesi kutoka Kisima cha Kiliwani  kilichopo katika Kitalu cha Kiliwani Kaskazini kinachomilikiwa na Ndovu Resources.

Dkt. Mataragio alisema kwa kuanzia mitambo itapokea kiasi cha futi za ujazo milioni moja kwa siku (1mmscfd) na kiasi hiki kitaendelea kukua hadi kufikia futi za ujazo milioni sabini kwa siku (70mmscfd). Kwa kiwanda cha Songo Songo kuanza kuzalisha gesi inamaanisha kwamba miundombinu ya kuchakata na kusafirisha gesi kutoka Madimba na Songo Songo imekamilika kwa asilimia 100%.

No.1(1)

Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt James Mataragio (katikati wenye kufungua valvu) akifungua valvu kwa pamoja na Mkandarasi kutoka CPTDC na Mshauri wa mradi kutoka Worley Parsons kuruhusu gesi kutoka kisima cha Kiliwani 1 kuelekea mitambo ya kuchakata gesi ya Songo Songo.

No.2

Moto (flare) ukionekana katika runinga kuashiria kuingia kwa gesi katika mitambo ya kuchakata gesi ya Songo Songo.

No.3(3)

Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio katika picha ya pamoja na watumishi wa Gasco, Wakandarasi wa CPTDC na  Mshauri mwelekezi kutoka Worley Parsons baada ya tukio la kuingiza gesi kutoka kisima cha Kiliwani 1 kuingia mitambo ya kuchakata gesi ya Songo Songo. Moto unaoonekana kwa nyuma unaashiria kuingia kwa gesi katika mitambo ya kuchakata gesi ya Songo Songo.

No.1

TPDC Yachangia Madawati 500 Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara

Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara imepokea jumla ya madawati  500 kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC). Akiongea wakati wa kupokea madawati hayo, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Bi. Halima Dendego alisema msaada huu unamaliza kabisa tatizo la madawati kwa kata zote za kijiji cha Madimba na Msimbati. Nae Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio alisema kwamba TPDC itaendelea kutoa misaada katika maeneo ambayo inafanya shughuli zake lengo likiwa ni kuboresha maisha wa wananchi wa maeneo hayo na kufaidika na shughuli za utafiti na uendelezaji wa gesi na mafuta.

No.1

Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio akikabidhi rasmimadawati 500 kwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Bi. Halima Dendego.

No.2

Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Bi. Halima Dendego na Mbunge wa Mtwara Vijijini. Mhe. Hawa Ghasia wakifurahia kwa pamoja baada ya TPDC kukabidhi madawati kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara.

No.3(2)

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Madimba wakiwa wamekaa katika madawati waliyopokea kutoka TPDC.

No.4(3)

Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio akionesha moja ya jezi ambayo TPDC ilitoa msaada kwa timu ya Wazawa FC iliyopo kijiji cha Mngoji, na Tagesh Academy zote za Mtwara.

No.1

Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara yapokea tozo ya kwanza ya gesi

No.1

Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio (mwenye miwani ya jua) akikabidhi mfano wa hundi ya Tsh. 150,000,000/ kwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Bi. Halima Dendego , Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Bi. Fatma Ally, Mbunge wa Mtwara Vijijini, Mhe. Hawa Ghasia na viongozi wengine wa Halmashauri wa Wilaya ya Mtwara.

 

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limelipa tozo ya kwanza ya huduma (Service Levy) inayotokana na shughuli za kuzalisha, kuchakata na kusafirisha gesi asilia kutoka Madimba hadi Dar es Salaam. TPDC imelipa kiasi cha Tshs. 150,000,000 ikiwa ni tozo ya huduma kwa shughuli za kuzalisha, kuchakata na kusafirisha gesi kuanzia mwezi Oktoba 2015 hadi Machi 2016 (miezi sita). Kiasi hiki kinajumuisha pia fedha kutoka Kampuni ya Maurel and Prom Tanzania Ltd ambayo ni wazalishaji wa gesi katika kitalu cha Mnazi Bay kilichopo kijiji cha Msimbati, Mtwara.

Akiongea wakati wa kukabidhi mfano wa hundi kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara, Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Dkt. James Mataragio alisema malipo ya tozo ya huduma yatakua yakifanywa kwa kipindi cha miezi mitatu mitatu ili kuwezesha Halmashauri kutekeleza mipango yao ya maendeleo bila kukwama.