VIONGOZI WA TPDC NA KAMPUNI ZAKE TANZU WAFANYA KIKAO KAZI

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limekutanisha Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika lake pamoja na Bodi za Usimamizi (Governing Bodies) za Kampuni zake Tanzu (GASCO na TANOIL) chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Balozi Ombeni Sefue, katika kikao cha pamoja kwa lengo la kufanya tathmini ya kina katika kuboresha utendaji kazi. Kikao hicho kilihudhuria pia na Menejimenti ya TPDC.Aidha, kikao kilifanyika Jijini Arusha.