WAZIRI MKUU AIPONGEZA TPDC KWA JUHUDI ZA USAMBAZAJI WA NISHATI SAFI

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), amelipongeza Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kwa juhudi zake katika kuhakikisha wananchi wa mikoa mbalimbali nchini, hususan Kanda ya Ziwa, wananufaika na nishati safi ya gesi asilia. Akizungumza katika banda la TPDC kwenye Kongamano la 4 la Tathmini, Ufuatiliaji na Mafunzo linalofanyika mkoani Mwanza, Mhe. Majaliwa amesema hatua zinazochukuliw...