TPDC YAANZA SURA MPYA YA UTAFUTAJI WA MAFUTA NA GESI ASILIA, YAPATIWA LESENI NNE

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limepiga hatua muhimu katika kuimarisha ushiriki wake wa moja kwa moja katika utafutaji wa mafuta na gesi asilia, baada ya Serikali kusaini leseni nne za utafutaji katika vitalu vya Mnazi Bay North, West Songo Songo, Eyasi-Wembere na Lindi-Mtwara. Hafla ya utiaji saini wa leseni hizo imefanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam, ikishuhudiwa...




