WAZIRI WA NISHATI AFANYA ZIARA FUPI TPDC

Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius John Ndenjembi amefanya ziara fupi katika Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) tarehe 24/11/2025 na kukutana na Bodi ya Wakurugenzi pamoja na Menejimenti ya Shirika hilo kwa madhumuni ya kufahamiana na kuweka misingi imara katika utekelezaji wa majukumu ya sekta ya mafuta na gesi nchini. Akizungumza katika kikao hicho, Waziri Ndenjembi aliipongeza TPDC kwa hatua mbalimbali za kimkakati ilizochukua...




