Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Aitaka TPDC Kuimarisha Uwekezaji katika Gesi Asilia

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughulikia Mafuta na Gesi, Dkt. James Mataragio, ameielekeza Menejimenti ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kuimarisha uwekezaji katika sekta ya gesi asilia kwa kuongeza vitalu vipya vya uwekezaji ili kuvutia wawekezaji zaidi katika shughuli za utafutaji na uzalishaji wa mafuta na gesi nchini. Dkt. Mataragio alitoa maelekezo hayo alipofanya ziara katika ofisi za TPDC jijini Dar es Salaam n...




