Mradi wa Utafutaji Mafuta wa Eyasi Wembere ni Kielelezo cha Ubora na Ufanisi wa TPDC

Mradi wa Utafutaji Mafuta wa Eyasi Wembere unaendelea kuwa kielelezo cha ubora, ufanisi na uwezo wa kitaalamu ambao Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania limeujenga katika sekta ya utafutaji wa mafuta na gesi asilia nchini. Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara ya ukaguzi wa mradi huo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TPDC, Balozi Ombeni Sefue, alisema tangu kuanza kwa shughuli za utafiti mwaka 2015 hadi sasa, TPDC imetumia...




