Tanga Kuwa Kitovu cha Nishati cha Kikanda

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, na Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni, leo wameshuhudia utiaji saini wa Hati ya Makubaliano (MoU) kati ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Kampuni ya Taifa ya Mafuta ya Uganda (UNOC) na Kampuni ya Vitol Bahrain kuhusu kuendeleza Mkoa wa Tanga kuwa Kitovu cha Nishati cha Kikanda. Hafla hiyo imefanyika katika Viwanja vya Ikulu, Dar e...




