MRADI WA EACOP WAANDIKA HISTORIA MPYA YA MAENDELEO AFRIKA MASHARIKI

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Mhe. Balozi Ombeni Sefue amesema kuwa Mradi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) ni miongoni mwa miradi bora zaidi duniani inayotekelezwa kwa kuzingatia utu haki za binadamu na uhifadhi wa mazingira. Akizungumza Jijini Tanga mbele ya Waandishi wa Habari Balozi Sefue amesema kuwa mradi huo unaotekelezwa kutoka Kabaale chini Uganda ha...