Mradi wa Gesi Asilia Kimiminika (LNG) wa Tanzania

Mradi huu unatekelezwa kufuatia kugundulika kwa kiasi kikubwa cha gesi takribani futi za ujazo 47.13 kwenye kina kirefu cha bahari katika mabonde ya bahari ya Tanzania, katika kitalu namba 1, 2, na 4. Kugundulika kwa gesi hii kulifanywa na Equinor katika kitalu namba 2 na Shell katika vitalu namba 1 na 4.
Watekelezaji wa mradi wa gesi wamemaliza kuchimba visima vya tathmini na sasa wako tayari kuanzisha majadiliano ya kibiashara, kiufundi, kisheria na kiudhibiti na Serikali kuhusu jinsi ya kutumia gesi iliyogundulika kupitia mradi wa LNG.
Tanzania iko kimkakati ili kunufaika na masoko ya mradi wa LNG katika Asia ya Kusini Mashariki, India, na Ulaya. Gesi ya Tanzania ni ya ushindani katika ubora kwani ina kiwango cha chini sana cha CO2, hivyo kuifanya kuwa nishati safi.