“Nimeridhishwa na utendaji kazi wa TPDC, hususan mchango wake katika kuhakikisha upatikanaji endelevu wa gesi asilia kwa ajili ya umeme, viwanda, usafiri na matumizi ya majumbani. Pia nalipongeza Shirika kwa kutekeleza kwa mafanikio jukumu la kuwa mwagizaji pekee wa mafuta katika kipindi hiki cha mpito,” alisema Mhe. Deogratius John Ndejembi.