DC MWAIPAYA ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MRADI WA UTAFUTAJI MAFUTA NA GESI ASILIA KITALU CHA LINDI-MTWARA

Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Mhe. Abdallah Mwaipaya, ameridhishwa na maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa utafutaji wa mafuta na gesi asilia katika Kitalu cha Lindi-Mtwara, unaotekelezwa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC). Mhe. DC Mwaipaya alieleza kuridhishwa huko baada ya kutembelea na kukagua maendeleo ya mradi huo, akisisitiza namna TPDC inavyotumia teknolojia ya kisasa ya mitetemo (3D Seismic) katika shughuli zake. "U...








