Category Archives: Uncategorized

Utekelezaji wa mradi wa kuunganisha gesi asilia kwa matumizi ya majumbani washika kasi

Dar es Salaam, 30 Julai 2018

Ni miezi mitatu sasa tangu Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani alipozindua rasmi mradi wa kuunganisha bomba kubwa la gesi asilia linalotoka Mtwara hadi Dar es Salaam na bomba la kipenyo kidogo linalotoka Ubungo kuelekea Mikocheni. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Mha. Kapuulya Musomba alifafanua kwamba utekelezaji wa mradi huo unalenga kuongeza matumizi ya gesi asilia kwa jiji la Dar es Salaam kwa kuwaunganisha wateja zaidi wa matumizi ya majumbani na viwandani.

Mradi huu unahusisha ujenzi wa msingi kwa ajili ya kusimika mtambo wa kupunguza mgandamizo, uunganishaji wa vipande vya mabomba, kuthibitisha njia ya bomba, uchimbaji na ulazaji wa bomba litakalochukua gesi kutoka bomba kubwa, uwekaji wa viainisho vya bomba linapopita na ujenzi wa daraja la waenda kwa miguu kuvuka mto Ubungo. Akizungumza juu ya hatua za utekelezaji, Meneja Mradi Ndg. Denice Byarushengo alisema “mradi umepiga hatua kubwa na muhimu ambapo hadi sasa ujenzi wa msingi kwa ajili ya kusimika mtambo wa kupunguza mgandamizo umekamilika kwa asilimia 97%, uthibitisho wa njia ya bomba na zoezi la kuchimba mitaro kwa ajili ya mabomba umekalimilika kwa asilimia 76.8%, uunganishaji wa mabomba umekamilika kwa asilimia 88.6%, ulazaji na ufukiaji wa mabomba umekamilika kwa asilimia 56.9%, viainisho sita (6) vya bomba linapopita vimeshawekwa na ujenzi wa dara la waenda kwa miguu umekamilika kwa asilimia 90%”. Aidha, Meneja Mradi aliongeza kwamba utekelezaji wa mradi huu unahusisha kuvuka mto Ubungo pamoja na barabara ya Ubungo Maziwa na ya Mandela ambapo hadi sasa kazi ya kuvuka mto Ubungo imekamilika kwa asilimia 100% na ile ya kuvuka barabara ya Ubungo Maziwa imekamilika kwa asilimia 50% wakati ya kuvuka barabara ya Mandela ikiwa mbioni kuanza.

Bomba lenye kipenyo cha 315mm likiwa limelazwa katika mtaro tayari kufukiwa, hii ni sehemu ya bomba linalochukua gesi asilia kutoka kwenye bomba kuu linalotoka Mtwara hadi Dar es Salaam na kuunganisha na bomba linalotoka Ubungo kuelekea Mikocheni.
Bomba lenye kipenyo cha 315mm likiwa limelazwa katika mtaro tayari kufukiwa, hii ni sehemu ya bomba linalochukua gesi asilia kutoka kwenye bomba kuu linalotoka Mtwara hadi Dar es Salaam na kuunganisha na bomba linalotoka Ubungo kuelekea Mikocheni.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Mha. Kapuulya Musomba ambaye alifanya ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya mradi huo hapo jana alionyesha kuridhishwa na kazi na ubora wa utekelezaji wa mradi, Mha. Kapuulya alisema “pamoja na changamoto zilizopo, ninayo furaha kwamba kazi zinafanyika kwa kasi na ubora wa hali ya juu na ni matumaini yangu baada ya kuongea na mkandarasi pamoja na msimamizi wa mradi kwamba mradi utamalizika ndani ya wakati”.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Mha. Kapuulya Musomba (mwenye overall ya bluu) akijadiliana jambo na Ndg. Ildefons Mnimbo ambaye ni mtaalamu kutoka kampuni ya Plasco anaesimamia zoezi la kuunganisha mabomba, alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa kuunganisha bomba kubwa la gesi kutoka Mtwara na lile la kutoka Ubungo kuelekea Mikocheni.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Mha. Kapuulya Musomba (mwenye overall ya bluu) akijadiliana jambo na Ndg. Ildefons Mnimbo ambaye ni mtaalamu kutoka kampuni ya Plasco anaesimamia zoezi la kuunganisha mabomba, alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa kuunganisha bomba kubwa la gesi kutoka Mtwara na lile la kutoka Ubungo kuelekea Mikocheni.

Mradi wa kuunganisha bomba kubwa la gesi asilia na lile la Ubungo kuelekea Mikocheni lenye urefu wa kilomita 7.8 na uwezo wa kusafirisha gesi kiasi cha futi za ujazo milioni 7.5 kwa siku unalenga kuunganisha kiwanda cha Coca Cola Kwanza Ltd na BIDCO pamoja na wateja takribani 1000 wa majumbani ambao wataunganishwa kwa awamu. Mradi huu utawezesha upatikanaji wa gesi asilia ya kutosha katika bomba litokalo Ubungo kuelekea Mikocheni kupitia barabara ya Sam Nujoma kusambaza gesi kwa wateja wa majumbani katika maeneo ya Ubungo, Shekilango, Mlalakuwa, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Sinza na Mikocheni. Mkandarasi wa mradi huu ni kampuni ya SINOMA kutoka Jamhuri ya Watu wa China na mradi unagharimu shilingi za kitanzania bilioni 4.2 ambazo ni fedha za ndani kutoka TPDC. Vile vile mradi huu unatoa fursa kwa kampuni za wazawa kutoa huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuuza bidhaa za ujenzi kama vile mabomba ambapo kwa sasa kampuni ya Plasco ndio mshindi zabuni hiyo. Mkandarasi wa mradi pia ana fursa ya kutoa kazi kwa mkandarasi mwingine (sub-contracting) lengo likiwa ni kuchochea ushirikishwaji wa wazawa katika sekta ya mafuta na gesi hapa nchini.

Sehemu ya eneo la barabara ya Ubungo Maziwa inayochimbwa kitaalamu bila kuvunja barabara ili kuruhusu bomba la gesi kuvuka barabara hiyo.
Sehemu ya eneo la barabara ya Ubungo Maziwa inayochimbwa kitaalamu bila kuvunja barabara ili kuruhusu bomba la gesi kuvuka barabara hiyo.
Meneja wa Kiwanda cha Kuchakata gesi asilia kinachomilikiwa na TPDC,Mhandisi Leonce Mrosso akiwaleza waheshimiwa Wabunge namna kiwanda hicho kinavyofanya kazi

Ziara ya Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Bajeti katika Miundombinu ya Gesi Asilia katika Mikoa ya Lindi na Mtwara

Bw. Laurent Jars-Meneja Uendeshaji wa KIwanda cha Kuchakata Gesi Asilia cha Maurel and Prom kilichopo Mnazi Bay Mkoani Mtwara akitoa maelezo kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Bajeti namna Kiwanda hicho kinavyofanya kazi
Bw. Laurent Jars-Meneja Uendeshaji wa KIwanda cha Kuchakata Gesi Asilia cha Maurel and Prom kilichopo Mnazi Bay Mkoani Mtwara akitoa maelezo kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Bajeti namna Kiwanda hicho kinavyofanya kazi.
MTWARA 1A
Bw. Laurent Jars akiendelea kutoa maelezo ya uendeshaji wa shughuli za uchakataji wa Gesi Asilia kiwandani
Mhandisi Felix Nanguka (kushoto) akifafanua jambo kwa Waheshimiwa Wabunge wa Kamati kuhusu Kisima cha gesi asilia (hakipo pichani) wakati Kamati hiyo ilipofanya ziara yake Mkoani Mtwara kukagua Miradi ya gesi asilia
Mhandisi Felix Nanguka (kushoto) akifafanua jambo kwa Waheshimiwa Wabunge wa Kamati kuhusu Kisima cha Gesi Asilia (hakipo pichani) Mkoani Mtwara
Meneja wa Kiwanda cha Kuchakata gesi asilia kinachomilikiwa na TPDC,Mhandisi Leonce Mrosso akiwaleza waheshimiwa Wabunge namna kiwanda hicho kinavyofanya kazi
Meneja wa Kiwanda cha Kuchakata gesi asilia kinachomilikiwa na TPDC,Mhandisi Leonce Mrosso akiwaleza waheshimiwa Wabunge namna kiwanda hicho kinavyofanya kazi

MTWARA 2

1

TPDC Kushirikiana na Kampuni ya Kitanzania

1

 

Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio (kushoto) na Mkurugenzi wa Minjingu, Bw. Pardeep Hans wakipeana mikono mara baada ya kutiliana sahihi Mkataba wa Makubaliano (MoU) katika utafiti wa mafuta na gesi na kufanya tathimini za kina katika Kitalu cha Songo Songo Magharibi.

 

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na Kampuni ya MINJINGU Mines & Fertliser Ltd ya Arusha wametia sahihi Hati ya Makubaliano (MoU) kushirikiana katika kufanya tathimini za kina katika kitalu cha Songo Songo Magharibi.

Akiongea baada ya kutia sahihi hati hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio alisema makubaliano kati ya TPDC na Kampuni ya Minjingu yanafungua fursa ya kufanya tathmini za kitaalamu kwa pamoja juu ya takwimu zilizopo za kitalu cha Songo Songo Magharibi ambacho kinamilikiwa na TPDC nia ikiwa ni kutafuta mashapo ambayo yanaweza kuhifadhi mafuta au gesi asilia.

“TPDC tayari ina takwimu nyingi kuhusu Kitalu cha Songo Songo Magharibi na itafanya kazi kwa karibu na Kampuni ya MINJINGU kuhakikisha kunakua na mafanikio katika mradi huu” amesema Dkt Mataragio.

Dkt. Mataragio amesisistiza kuwa makubaliano hayo yanatoa wajibu kwa pande zote mbili kufanya kazi kwa pamoja ndani ya kipindi cha mwaka mmoja kutathmini uwezekano wa mashapo ya kitalu cha Songo Songo Magharibi kuhifadhi mafuta au gesi.

“Iwapo kutakua na matokeo chanya basi hatua zingine za utafiti ikiwemo kuchimba kisima zitafuata” aliongezea Dkt. Mataragio.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Minjingu, Ndugu Pardeep Hans alisema wao kama kampuni ya kizawa wamefurahi sana kuaminiwa na Serikali na watafanya kazi kwa weledi wa hali ya juu wa kushirikiana na TPDC ili kuhakikisha wanafikia lengo la ushirikiano wao.

“Endapo gesi itagundulika basi itatumika kutumika katika mradi wa mbolea ambao MINJINGU wako ubia na TPDC” pamoja na Ferrostaal kutoka Ujerumani, Haldor Topsoe ya Denmark na Fauji ya Pakistani” alisema Bw. Hans.

Makubaliano hayo ya awalia yanafungua fursa ya TPDC pamoja na MINJINGU ya ushirikiano wa utafiti katika Kitalu cha Songo Songo Magharibi, Kampuni ya Mijingu ikiwa Kampuni ya kwanza ya Kizawa kushirikiaa na TPDC katika utafiti wa mafuta na gesi.

 

1

TPDC yawakutanisha wadau wa mradi wa “LNG” DAR

1

Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Prof. James Mdoe akifungua warsha ya siku mbili kwa Wadau wa Mradi wa kusindika gesi asilia nchini (LNG) jijini Dar es Salaam.

 

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) katikati ya juma liliandaa warsha ya siku mbili ya Wadau wa Mradi wa kusindika gesi asilia kuwa kimiminika kwa ajilia ya kusafirisha nje ya nchi na matumizi ya nchini (LNG).

Akifungua Warsha hiyo kwa Niaba ya Waziri wa Nishati na Madini, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Prof. James Mdoe alisema warsha hiyo inalenga kuwakutanisha wadau wanaoshiriki katika utekelezaji wa Mradi huo.

“Warsha hii pia imekusudia kutengeneza mazingira shirikishi kwa wadau hao kabla ya kuanza kutekeleza ujenzi wa Mradi huo” alisema Prof. Mdoe.

Alisema msukumo mkubwa wa Taifa kwa sasa ni kuelekea kuwa nchi ya viwanda na kichocheo kikubwa cha kufikia lengo hili ni matumizi ya rasimali ya gesi kutumika kama nishati.

“Ni shauku yangu kwa sasa ni kuona Tanzania inavyojivunia fursa za uwekezaji hususani katika tasnia ya gesi asilia”, alisema Prof. Mdoe.

Hata hivyo alisema kufuatia kuwepo kwa gesi yakutosha kutasukuma utekelezaji mradi wa Mradi wa kusindika gesi asilia nchini.

Aliongeza kuwa ushirikishwaji wa wadau muhimu na elimu ndiyo makusudi makuu ya warsha hiyo kabla ya kuanza kutekelezwa kwa mradi huo.

Aidha, akufunga warsha hiyo kwa niamba ya Mkurungezi Mtendaji wa TPDC, Mkurugenzi wa Usafishaji, Usafirishaji na Usambazaji wa Gesi Asilia, Dk. Wellington Hudson alisema warsha hiyo ilikuwa ya mafanikio makubwa kwa kuwakutanisha wadu muhimu wa Mradi wa kusindika gesi asilia nchini.

Alisema licha ya kutarajiwa kujengwa kwa Kiwanda cha kusindika gesi asilia nchini kwa kusafirisha gesi asilia nje ya nchi pia gesi asilia itatumika kwa soko la nchini na Afrika Mashariki.

Aliongeza kuwa mada zilizo wasilishwa katika katika warsha hiyo zilikuwa na tija kubwa katika kuelekea utekelezaji wa Mradi huo.

Ujenzi wa Kiwanda cha kusindika gesi asilia kwa matumizi ya ndani na kusafirisha nje ya nchi unatarajiwa kujengwa eneo la Likong’o katika Manispaa ya Lindi na unatarajia kugharimu Dola za Kimarekani bilioni 40 hadi 60.

Warsha hiyo imewakutanisha wadau kutoka Wizara ya Nishati na Madini, TPDC, Taasisi kutoka Serikalini na Makapuni ya Wawekezaji ya Mafuta na Gesi Nchini.

1

Wanawake wa TPDC Washiriki Siku ya Wanawake Duniani

Machi 8 kila mwaka wanawake huadhimisha siku ya wanawake duniani, siku ambayo huadhimishwa pia na nchi wanachma wa Umoja wa Mataifa.
Mwaka huu wanawake wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) “Oil and gas women group” waliungana na wanawake wengine duniani kuadhimisha siku hiyo.
Walishiriki maadhimisho hayo yaliyo fanyika Kimkoa katika viwanja vya Biafra jijini Dar es Salaam, mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu.
Kaulimbiu ya mwaka huu ilikuwa “50/50 ifikapo 20-30 tuongeze jitihada”

1

 Wanawake wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) “Oil and gas women group” wakiwa katika maandamano kuelekea katika viwanja vya Biafra jijini Dar es Salaam.

2

Wanawake wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) “Oil and gas women group” katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.

3

Wanawake wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) “Oil and gas women group”.

4

Kauli mbiu ya TPDC

“Utawala bora na fursa zinazo ambatana na gesi asilia ni chachu ya kufikia 50/50 ifikapo 2030