TPDC-A1

SERIKALI ZA TANZANIA NA UGANDA ZAINGIA MAKUBALIANO NA KAMPUNI YA TOTAL E&P

Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio (kushoto), Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava, (wa pili kushoto), Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Nishati na Madini (Uganda) Dkt. Fred Kabagambe Kaliisa (wa pili kulia) na Meneja Mkuu wa Total E&P Uganda, Ndg. Adewale Fayemi (kulia). Kwa pamoja wakibadilishana nakala za Hati ya Makubaliano (MoU) baina ya Serikali ya Uganda na Tanzania juu ya utekelezaji wa mradi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Uganda (Kabaale) mpaka bandari ya Tanga (Tanzania).

 

Serikali Tanzania na Uganda zaingia makubaliano na Kampuni ya total E&P

Serikali za Tanzania na Uganda pamoja na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na kampuni Total E&P ya Uganda wametia saini hati ya makubaliano ya utekelezaji wa mradi wa kusafirisha mafuta ghafi kwa bomba kutoka Uganda kupitia Tanzania.
Tukio hilo limefanyika jiji la Kampala nchini Uganda huku Tanzania ikilishwa na Wizara ya Nishati na Madini pamoja na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania.
Akiongea baada ya kusaini Hati hiyo, Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava alisema Tanzania na Uganda wana historia ndefu ya ushirikiano na mradi huu utazidi kuboresha ushirika kati ya nchi hizi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Dkt. James Mataragio alisema kuwa TPDC ina uzoefu wa muda mrefu katika ujenzi, uendeshaji na utunzaji wa bomba na hivyo uzoefu huu utasaidia sana katika utekelezaji wa mradi huu.
Mradi huu wa kusafirisha mafuta ghafi kwa bomba kutoka Uganda hadi Tanzania endapo utakamilika utafungua fursa kwa serikali hizi mbili kufanya kazi kwa pamoja na kuangalia uwezekano wa kuendeleza uchumi wa inchi zote mbili.
Mradi huu wa kusafirisha mafuta ghafi kutoka kabaale Uganda kupitia Tanzania mpaka bandari ya Tanga utatoa faida nyingi ambazo zitapatikana kwa Tanzania na Uganda ambazo ni zaidi ya utekelezaji wa mradi huu.
Hata hivyo makubaliano haya yanatoa muongozo kwa pande zote zinazohusika kuendelea kufanya kazi kwa pamoja kuboresha tafiti zilizokwishafanyika juu ya njia ya bomba hilo.
Wakati huo huo wiki hii, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alifungua rasmi mradi wa bomba la gesi la kilometa 542 kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam unaomilikiwa na kuendeshwa na TPDC.

TPDC-1

JK AZINDUA MRADI WA GESI ASILIA MTWARA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea taarifa fupi ya kiwanda cha kuchakata gesi asilia eneo la Madimba Mkoani Mtwara kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio (kulia) kabla ya kuzindua kiwanda hicho, katikati ni Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene.

2

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizindua kiwanda cha kuchakata gesi asilia eneo la Madimba Mkoani Mtwara mwishoni mwa wiki.

3

Rais Kikwete akipatiwa maelezo ya jinsi kiwanda cha kuchakata gesi asilia kinavyofanyakazi kutoka kwa Mhandisi, Sultan Pwaga, kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio.

4

Wageni mbalimbali na wananchi walio hudhuria uzinduzi huo.

5

Sehemu ya kiwanda cha kuchakata gesi asilia Madimba Mkoani Mtwara kilizichozinduliwa na Rais Kikwete .

6

Kiwanda cha kuchakata gesi asilia kilichoko Madimba Mkoani Mtwara.

MD-TPDC

RAIS KIKWETE KUZINDUZUA MIUNDOMBINU YA GESI ASILIA

Miundombinu ya kuchakata na kusafirisha gesi asilia kutoka Mtwara na Songo Songo mpaka Dar es Salaam kupitia Somanga inatarajiwa kuzinduliwa na Mh. Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete tarehe 10 Oktoba, 2015 eneo la Madimba Mkoani Mtwara.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) Tanzania Dkt. James Mataragio alieleza kuwa miundombinu hiyo imekamilika na tayari gesi imeshaanza kusukumwa kutoka Mtwara mpaka Dar es Salaam.
Dkt. Mataragio alisema mandaalizi ya uzinduzi yanaendelea na yako katika hatua za mwisho za maadalizi ya kufanikisha shughuli hiyo.
“kwa upande wa Mtwara ambapo tayari gesi imeanza kusukumwa kutoka Mtwara tayari kiasi cha futi za ujazo za milioni 60 zinasukumwa kwa siku, kiasi hiki cha gesi kinazalishwa na visima vitatu ambavyo kila kimoja kinazalisha futi za ujazo milioni 20” alisema Dkt. Mataragio.
Aliongezea kuwa mpaka ifikapo mwishoni mwezi Oktoba kisima cha nne ambacho kitakuwa kikizalisha futi za ujazo cha milioni 20. Pindi kisima hiki kitakavyokamilika gesi itokayo madimba itafikia futi za ujazo milioni 80 kwa siku.
Mkurugezi Mtendaji alisisitiza gesi asilia iliyogunduliwa ipo nyingi haswa iliyopo baharini na kwamba mradi huu kwa sasa utatumia gesi ya nchi kavu.
“Manufaa ya gesi asilia ni kama vile upatikanaji wa umeme wa uhakika katika gridi ya Taifa, ukuaji wa sekta ya viwanda kutokana na upatikanaji wa nishati ya uhakika na mali ghafi za viwandani kama mbolea na plastiki, ukuaji wa pato la taifa na kuongeza upatikanaji wa ajira’’ Dkt. Mataragio alifafanua.
Dkt. Mataragio, aliwaalika wananchi wote haswa wa mikoa ya Lindi na Mtwara kuhudhuria sherehe za uzinduzi huo.