1

NDEGE YA UTAFITI WA MAFUTA NA GESI YATUA KILIMANJARO

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Dkt. James Mataragio akuzungumza mbele ya waandishi wa habari kuhusu ujio wa ndege ya pili ya utafiti wa awali wa mafuta na gesi asilia katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) mwishoni mwa wiki, ndege hiyo inatarajia kuanza utafiti wiki hii katika kitalu cha Eyasi Wembere na Mandawa.

2

Mkurugenzi Mtendaji TPDC Dkt. James Mataragio akipatiwa maelekezo ya jinsi ndege hiyo inavyofanya kazi (ndani ya ndege) kutoka kwa Meneja wa Mradi Brett Robinson wa kampuni inayoendesha utafiti huo ya “CGG AVITION LTD” katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), utafiti huo unagharamiwa na TPDC kutoka katika mfuko wa fedha za maendeleo.

3

Ndege ya utafiti wa awali wa mafuta na gesi asilia inayotarajia kuanza utafiti katika kitalu cha Eyasi Wembere na Mandawa ikiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) Mkoani Kilimanjaro mwishoni mwa wiki.

5

Meneja wa Mradi Brett Robinson wa kampuni inayoendesha utafiti huo ya “CGG AVITION LTD” (kushoto) akitoa ufafanuzi mbele ya waandishi wa habari jinsi ndege hiyo itakavyofanya utafiti, Mkurugenzi Mtendaji TPDC Dkt. James Mataragio (kulia).

6

Mratibu wa Mradi kutoka TPDC, Ndg. Sindi Maduhu, akielezea njinsi wataalamu kutoka TPDC watakavyo shirikiana na kampuni inayoendesha utafiti huo ya “CGG AVITION LTD” kufanikisha utafiti huo.