1

Wanawake wa TPDC Washiriki Siku ya Wanawake Duniani

Machi 8 kila mwaka wanawake huadhimisha siku ya wanawake duniani, siku ambayo huadhimishwa pia na nchi wanachma wa Umoja wa Mataifa.
Mwaka huu wanawake wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) “Oil and gas women group” waliungana na wanawake wengine duniani kuadhimisha siku hiyo.
Walishiriki maadhimisho hayo yaliyo fanyika Kimkoa katika viwanja vya Biafra jijini Dar es Salaam, mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu.
Kaulimbiu ya mwaka huu ilikuwa “50/50 ifikapo 20-30 tuongeze jitihada”

1

 Wanawake wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) “Oil and gas women group” wakiwa katika maandamano kuelekea katika viwanja vya Biafra jijini Dar es Salaam.

2

Wanawake wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) “Oil and gas women group” katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.

3

Wanawake wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) “Oil and gas women group”.

4

Kauli mbiu ya TPDC

“Utawala bora na fursa zinazo ambatana na gesi asilia ni chachu ya kufikia 50/50 ifikapo 2030

No.1

WAZIRI MKUU ATEMBELEA KIWANDA CHA KUCHAKATA GESI, MADIMBA-MTWARA

 

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa (MB) mwishoni mwa juma alifanya ziara katika mitambo ya kuchakata gesi asilia iliyopo Madimba, Mtwara. Katika ziara hiyo, Mh. Majaliwa aliweza kujionea uwekezaji wa kimataifa uliofanywa na Serikali kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanznaia (TPDC). Akiongea wakati wa ziara hiyo, Mh. Majaliwa alisema “nawapongeza sana kwa kazi nzuri mnayoifanya, ni jambo la fahari kuona Watanzania wakiendesha mitambo hii tena kwa umakini mkubwa”. Akiwa kiwandani hapo, Mh. Majaliwa aliweza kuzungumza na watumishi wa TPDC na kuwataka kuendelea kuchapa kazi kwa kutumia utaalam wao na kutambua kwamba Taifa linawategemea. Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio alieleza juhudi za TPDC kuuelimisha umma kuhusu sekta ndogo ya gesi na mafuta ili kuwaandaa wananchi na fursa zilizopo na zinazokuja na miradi mikubwa ya gesi.

No.1

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa (MB) akipokea maelezo kutoka kwa Meneja wa Kiwanda cha Kuchakata gesi-Madimba, Mhandisi, Sultan Pwaga, wengine ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dr. Medard Kalemani (Kulia kwa Waziri Mkuu) na Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Dkt. James Mataragio (kushoto kwa Waziri Mkuu)

No.2

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa (MB) akimsikiliza kwa makini Ndugu Stanslaus Mallya (mwenye nguo nyekundu) akitoa maelezo namna ya kuendesha mitambo kutokea chumba cha uendeshaji (Control Room)

No.3

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa (MB) akifurahia jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio, wengine ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dr. Medard Kalemani na Mbunge wa jimbo la Mtwara Vijijini, Mh. Hawa Ghasia

No.4

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa (MB) akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya TPDC pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Bi Halima Dendego (Kushoto kwa Waziri Mkuu).