Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limekabidhi rasmi Karakana ya Kisasa ya kuongeza mfumo wa matumizi ya Gesi Asilia Iliyoshindiliwa (CNG Conversion Workshop) kwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), hatua inayolenga kuimarisha matumizi ya nishati safi nchini pamoja na kukuza wataalamu wa teknolojia ya gesi asilia.