1

TPDC Yawashika Mkono Wana-Kagera

1Kaimu Mkurugenzi wa TPDC Mhandisi, Kapuulya Musomba (kulia) akiwa amemshika mkono Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu mara baada ya kukabidhi msaada wa vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya shilingi milioni ishirini (20,000,000) kwa waathirika wa tetemeko Mkoani Kagera.

Kufuatia hali inayoukabili mkoa wa Kagera kutokana na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani humo mnamo septemba 10 mwaka huu na kusababisha maafa makubwa kwa baadhi ya Wananchi na hata kuchukua uhai wa watu 17 Mkoani humo

Shirika la Maendeleo ya Petrol Tanzania (TPDC) limeungana na jitihada za Serikali katika kusadia waathirika wa tetemeko Mkoani humo kwa kutoa vifaa vya ujenzi ikiwa ni pamoja na saruji na mabati vyenye thamani ya shilingi millioni 20 kwa ajili ya kusaidia ujenzi kwa walioguswa na maafa hayo.

Baada ya kukabidhi vifaa hivyo kwa Mkuu wa Mkoa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji TPDC Mhandisi, Kapuulya Musomba amesema kuwa wametoa vifaa hivyo vyenye thamani ya shilingi millioni 20 kwa ajili ya kuwasadia waathirika wa tetemeko hilo.

Pia Mhandisi Musomba amesema kuwa misaada waliotoa sio mwisho badala yake watahakikisha wanaendelea kuwafuatilia kampuni washirika wanaofanya kazi na TPDC nchini, huku akiongeza kuwa tayari wameshawaandikia barua ya kuwaomba kuchangia na kushiriki katika kusaidia Wanakagera.

0

Makamu wa Rais Atembelea Mitambo ya Kuchakata Gesi Asilia Madimba, Mtwara

 

0

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa mitambo ya kuchakata gesi asilia iliyopo Kijiji cha Madimba, Mkoani Mtwara, Ndugu Leoce Mrosso (wapili kushoto) wakati wa ziara yake Madimba Mkoani Mtwara.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya ziara kutembelea mitambo ya kuchakata gesi asilia ya Madimba iliyoko Mkoani Mtwara. Ikiwa ni miezi 11 tu tangu Rais wa awamu ya nne kuzindua mitambo hiyo, mchango wake katika upatikanaji wa umeme wa uhakika ni wa hali ya juu ambapo hadi sasa takribani megawati 400 za umeme zinazalishwa kwa gesi asilia inayochakatwa katika mitambo hii.

Akiongea baada ya kutembelea miundombinu hiyo, Makamu wa Rais alisema “ ni vema TPDC ikatambua kwamba imebeba moyo wa Serikali ambapo ili kufikia dhamira ya Serikali ya kuwa na uchumi wa viwanda, nishati ni kitu cha msingi katika kufikia lengo hilo”.

Vile vile, Makamu wa Rais aliwapongeza watumishi wa TPDC kwa kazi nzuri wanayofanya na kusisitiza kwamba mcheza kwao hutuzwa.

Nae Naibu Katibu Mkuu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Prof. James Mdoe alitoa taarifa fupi ya mradi ambapo alieleza pamoja na mambo mengine namna ambavyo mradi umesaidia kupunguza matumizi ya fedha za kigeni ambazo zilikua zinatumika kununua mafuta mazito kwa ajili ya kuzalisha umeme.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Mhandisi Kapuulya Musomba alieleza namna ambavyo TPDC inashirikiana na jamii ambazo zinazunguka maeneo ya miradi nia ikiwa ni kujenga mahusiano bora baina ya Shirika na jamii husika.