2

Shule ya Sekondari Kisungu ya Ilala Yapokea Viti Kutoka TPDC

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limekabidhi viti 142 vyenye thamani ya shilingi milioni 6 katika Shule ya Sekondari Kisungu iliyopo kata ya Kinyerezi jijini Dar es Salaam.

Meneja Mawasiliano wa TPDC, Marie Msellemu akikabidhi viti hivyo amesema viti hivyo vitasadia kutatua changamoto ya wanafunzi kukosa viti shuleni hapo.

Amengoze kuwa mchango huo wa viti ni kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika kuhakikisha wanafunzi wanakuwa na mazingira rafiki ya kujifunzia.

Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Sekondari Kisungu Mukama Mgeta ameshukuru msaada wa vitu kutoka TPDC na kwamba viti hivyo vitasaidia kupunguza changamoto ya upatikanaji viti shule hapo.

Shirika hilo limekuwa na utaratibu wa kuwajibika kwa jamii katika nyaja za afya, elimu, maji, utawala bora na michezo kupitia programu yake kuwajibika kwa jamii.

1

Meneja Mawasiliano wa TPDC, Marie Msellemu akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC katika hafla fupi ya kukabidhi viti 142 vyenye thamani ya shilingi milioni 6 katika kwa Shule ya Sekondari Kisungu iliyopo kata ya Kinyerezi jiji Dar es Salaam.

2

Mkuu wa shule ya Sekondari Kisungu, Mkama Mgeta (kulia) na wanafunzi wa Shule ya Sekondari wakipokea kiti kutoka kwa Meneja Mawasiliano wa TPDC, Marie Msellemu (kushoto) katika hafla fupi ya kupokea viti 142 kutoka TPDC.

3

Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari Kisungu, Philimina Casimr akisoma taarifa ya Shule hiyo kabla ya kupokea viti kutoka TPDC.

4

Sehemu ya viti 142 vilivyotolewa na TPDC

1

Kiwanda cha Vigae Mkuranga Kupatiwa Gesi

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Mdini Prof. Justin Ntalikwa (aliyevaa shati la kitenge) akioneshwa na Kaimu Mkurugenzi Mtaendaji wa Kampuni ya Goodwill, Robin Huang (aliyenyoosha mkono kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Mtaendaji wa TPDC (aliyenyoosha mkono kulia) eneo patakapo jengwa bomba la kuunganisha gesi katika kiwanda cha Goodwill cha kuzalisha vigae Wilaya ya Mkulanga Mkoani Pwa

 

Kaibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Prof. Justin Ntalikwa amesema kuwa serikali itaunganisha kuunganisha gesi asilia katika kiwanda cha vigae kilichopo Wilaya ya Mkuranga, Mkoani Pwani.

Alisema kiwanda cha Kampuni ya Goodwill inayoendelea na ujenzi wa Kiwanda hicho itaunganishiwa gesi na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) mara baada ya ujenzi kukamilika.

“Kiwanda hiki kinatarajia kuzalisha vigae kwa ajili ya shughuli mbali mbali za ujenzi na katika kuzalisha vigae hivyo Kampuni itahitaji gesi kwa ajili ya kuendesha mitambo na kuzalisha umeme wa megawati nane (8) kwa ajili ya kuendeshea kiwanda, alisema Prof. Ntalikwa.

Alisema kuwa kwa upande wa Wizara ya Nishati na Madini itahakikisha gesi inayohitajika wanapatikana, ili kutowakwamisha katika juhudi zao za uzalishaji.

“Sehemu ambayo gesi itaunganishwa iko karibu ni umbali wa chini ya kilomita moja, kwa maana hiyo kazi iliyopo nikujenga bomba dogo litakalo unganishwa na bomba kubwa la TPDC la nchi thelathini na sita (36),” alifafanua Ntalikwa.

Prof. Ntalikwa alisema kuwa ujenzi wa Kiwanda unatarajiwa kukamilika mwezi Desemba mwaka huu na zao la kwanza la kiwanda linatarajiwa kutoka mwezi januari mwakani.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Mhandisi Kapuulya Musomba alisema TPDC ikotayari kuona Serikali inafanikiwa katika malengo ya kuwa na viwanda na gesi inakuwepo kwa viwanda hivyo.

“Tumekuwa na mazungumzo mazuri na Kampuni ya Goodwill kwa ajili ya kuwaunganishia gesi katika Kiwanda chao na hatuo iliyopo ni kujenga bomba la kuunganishiwa gesi hiyo,” alisema Mhandisi Musomba.

Aliongeza kuwa Kiwanda cha Goodwill ni kiwanda cha kwanza kwa upande wa TPDC ambacho ndicho kitauziwa gesi ukiondoa Tanescio ambayo imekuwa ikiuziwa.

Aidha, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Goodwill, Robin Huang alisema kuwa matumizi ya nishati ya gesi asilia ni nafuu katika uendeshaji wa kiwanda.

“Tutatumia gesi asilia kama nishati kuu kwa ajili ya uzalishaji katika kiwanda chetu kwani ni nafuu kwa bei na tumepata ushirikiano mkubwa kutoka kwa Serikali” alisema Huang.

Gesi itakayo hitajika katika kiwanda hicho kwa kuanzia itakuwa futi za ujazo milioni 7 kwa siku, na baada ya miaka mitatu itafikia futi za ujazo milioni 10 kwa siku.

Kiwanda cha Goodwill kinatarajia kukamilika ujenzi wake mwezi Disemba na kuanza uzalishaji mwezi Januari 2016. Kiwanda hicho kitakuwa na uwezo wa kuzalisha mita za mraba 8,000 kwa siku.

Uzalishaji wa kiwanda hicho unategemea kuchukua sehemu kubwa ya soko la vigae vya ujenzi nchini, kwani kinatarajiwa kufungua matawi katika miji yote mikubwa chini.

2

Prof. Ntalikwa: Gesi Mtwara Ipo kwa Wawekezaji

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Prof. Justin Ntalikwa amesema kuwa kiwango cha gesi asili kilichopo Mtwara kinauwezo wa kutumika kwa viwanda vipya vya mbolea Mkoani Mtwara.

Prof. Ntalikwa amesema hayo mwishoni mwa juma katika ziara yake Mkoani Mtwara ya kujionea maeneo ya uzalishaji na utafiti wa gesi asilia Mkoani humo.

“tumejiridhisha kwamba kiasi cha gesi kitakachopatikana kinatosha kabisa kwa ajili ya kiwanda cha mbolea kinacho tarajiwa kujengwa Mkoani Mtwara,” alisema Prof. Ntalikwa.

Alisema kuwa katika eneo la Ntorya, Halimashauri ya Mtwara ambako Kampuni ya Ndovu Resources inaendesha utafiti wa gesi asilia tayari kumekwisha gundulika gesi na kinachofanyika sasa ni uhakiki wa hifadhi ya gesi hiyo.

“Kisima cha kwanza cha gesi kimekwisha gundulika kiasi cha gesi cha futi za ujazo trilioni 0.15,” alisema Prof. Ntalikwa.

Alifafanua kuwa, kisima cha pili kinatarajiwa kuchimbwa na kinakadiriwa kuwa na futi za ujazo trilioni 0.9, huku kisima cha tatu kikitarajiwa kuwa na futi za ujazo 1.5.

Alisema eneo jingine lilionekana kuwa na uwezekano wa kuzalisha gesi asilia ni eneo la Msimbati liliko Halimashauri ya Wilaya Mtwara.

“Kampuni ya Maurel and Prom (M & P) pia wameonyesha wako tayari watakapo hitajika kuchimba visima vingine kwa ajili ya uzalishaji kufanya hivyo,” aliongezea Prof. Ntalikwa.

Prof. Ntalikwa alisema kuwa kunatarajiwa kujengwa Kiwanda cha Mbolea cha Kampuni ya Helm ya Ujerumani Mkoani humo huku kihitaji kiasi cha gesi cha futi za ujazo 0.8 kwa kipindi cha miaka ishirini.

Alisisitiza kuwa maeneo hayo yote yanauwezo kwa kutoa gesi ya kutosha kwa ajili ya Kiwanda hicho cha mbolea na kwa kampuni nyingine zitakazo wekeza Mkoani humo.

Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Bi. Halima Ndendegu alishukuru kwa ziara ya Katibu Mkuu Mkoani Kwake kwa kuhakikisha upatikanaji wa gesi asilia kwa wawekezaji.

“Nimefarijika sana kwa hii ziara ya leo kwani katika ziara nzima mmeweza kuona wawekezaji walivyotayari kupokea miradi,” alisema Bi. Dendegu.

Aliongeza kuwa uhakika wa upatikanaji wa gesi ni hatua moja mbele katika kuhakikisha uwekezaji katika sekta ya viwanda unatokea Mkoani Mtwara.

“nimeridhishwa na zile taarifa za kitaalam ambazo nimezipata, lakini kubwa zaidi pale nilipoambiwa hata nikitaka gesi leo kama niko tayari na mwekezaji naweza nikapata,” asisitiza Bi. Dendegu.

Kwa upande waka, Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Mhandisi Kapuulya Musomba alisema kuwa TPDC inakazi kubwa ya kuhakikisha gesi inapatikana kwa ajili ya viwanda nchini.

“Kitendo cha watu kuwepo wanahitaji gesi kwetu sisi ni faraja kubwa na ndio kazi kubwa tunatakiwa tuifanye,” alisema Mahandisi Musomba.

Ameleza kuwa TPDC iko tayari kuona inashirikiana na wawekezaji ili kukidhi mahitaji ya viwanda ambavyo vinatarajiwa kujengwa Mkoani Mtwara.

“Ujio wetu hapa Mtwara ni kuhakikisha viwanda vitakavyojengwa Mtwara vya mbolea na kemikali vinapata gesi asilia,” aliongeza Mahandisi Musomba.

Kampuni ya Helm ya Ujerumani inatarajia kujenga kiwanda cha mbolea katika eneo la Msanga Mkuu lenye ukubwa wa hekta mianne (400), Mkoani Mtwara.