1

TPDC yachangia ukarabati wa Kituo cha Polisi Mtwara

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TPDC, Prof. Sufian Bukurra (wa pili kulia) akikabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni tano kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, George Salala (wa kwanza kushoto) kwajili ya ukarabati wa Kituo cha Polisi Uwanja wa ndege Mtwara, wengine ni Kaimu Mkurugenzi wa TPDC Mhandisi, Kapuulya Musomba (kwa kwanza kulia), Mkuu wa Mkuu wa Kituo cha Polisi Uwanja wa ndege Mtwara, Inspekta, Moses Moremi (wa pili kushoto) na Kaimu Meneja wa Uwanja wa ndege Mtwara, Vita Majinge (katikati).

Shirika la Mendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limekabidhi mchango wa ukarabati wa Kituo cha Polisi cha Uwanja wa Ndege Mtwara.

Akikabidhi mchango huo Mwenyekiti ya Bodi ya Wakurugenzi wa TPDC, Prof. Sufian Bukurura amesema mchango huo anamini utasadia kufanikisha ukarabati wa Kituo hicho unaoendelea.

“Mchango uliotolewa leo na TPDC ni mchango ambao unaweza kufungua fursa ya kuwaunganisha na wadau wengine wachangie zaidi’” alisema Prof. Bukurura.

Prof. Bukurura ameushukuru uongozi jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara kwa ushirikiano uliopo katika ya jeshi hilo na TPDC hususan katika ulinzi wa miondombinu ya gesi asilia Mkoani humo.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TPDC akiwa na wajumbe Bodi hiyo katika ziara ya kikazi Mkoani humo amekabidhi hundi ya shilingi milioni tano fedha zilizotolewa na TPDC kwa ajili ya ukarabati wa Kituo cha Polisi  Uwanja wa Ndege Mtwara.