Serikali imeamua kuipatia TPDC leseni zake binafsi za utafiti wa mafuta na gesi asilia, kufuatia kuimarika kwa uwezo wa Shirika katika kutekeleza shughuli za utafiti. Hapo awali, TPDC ilikuwa ikitekeleza shughuli hizo kwa kushirikiana na kampuni za kimataifa, lakini sasa imefikia hatua ya kuweza kuendesha tafiti kwa kutumia uwezo wake yenyewe.